Luke 22:41-44

41 aAkajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42 bakisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 43 cMalaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 dNaye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.

Copyright information for SwhKC